Ustar Wangu ni Nje ya Ndoa. :-Mwanakheri - Ghafla TZ | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Ustar Wangu ni Nje ya Ndoa. :-Mwanakheri

Mwanadada Mwanakheri amefunguka na kusema kuwa katika maisha yake ya uigizaji amekuwa akifanya ustae nje ya nyumbani kwake lakini akifika nyumbani kwake yeye ni mke wa mtu na wala sio staa tena.


Mwanakheri anasema kuwa mara nyingi amekuwa akijikumbusha kuwa endapo ataleta ustaa nyumbani inaweza kumharibia nyumba na familia yake na hata kuvunja ndoa kwa ujumla hivyo kila siku amekuwa akifikilia hilo.


Mwanakheri anasema kuwa amekuwa akijifunza inavyotokea kwa mastaa wengine na anaona kuwa kwake haiwezi kutokea kwa sababu mara zote amekuwa makini na swala hilo.


kikubwa ni kuwa nikimuomba sana Mungu kuhusu kuilinda ndoa yangu, lakini kikubwa pia ni kwamba niekuwa nikimheshimu sana mume wangu, nampenda na ninamhshimu sana na hivyo maisha yangu ya ndani ya ndoa ni tofauti na ya huko nje kabisa.


The post Ustar Wangu ni Nje ya Ndoa. :-Mwanakheri appeared first on Ghafla!Tanzania.... Continue reading ->


Source: Ghafla TZRead More