UTAFITI: Watoto wachanga 6 hufariki kila baada ya saa mbili - Kwanza TV | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

UTAFITI: Watoto wachanga 6 hufariki kila baada ya saa mbili

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, limesema, kila baada ya saa mbili mwanamke mmoja na watoto wachanga sita wanaozaliwa nchini Yemen wanafariki kutokana na matatizo wakati wa ujauzito au wakati wa kujifungua.


Takwimu hizo zimo kwenye mfululizo wa makala zinazoonesha kujifungua na kulea katika ukanda wa vita, zimezinduliwa wiki hii na pia zinaeleza kuwa tangu kuongezeka kwa mapigano, vifo wakati wa kujifunga vimeongezeka kwa kasi kutoka vifo vitano kwa siku mwaka 2013 na kufikia 12 kwa siku mwaka 2018.


Nyongeza ya matokeo ya utafiti inafafanua kuwa mwanamke mmoja kati ya wanawake 260, wanafariki dunia wakati wa ujauzito na wakati wa kujifungua. Halikadhalika  ni matukio matatu tu kati ya 10 ya kujifungua yanafanyika katika hospitali, kichanga kimoja katika ya vichanga 37 vinapoteza maisha katika mwezi wao wa kwanza wa maisha.


Utafiti huo pia umeeleza kuwa  vijana  wa kike mmoja kati ya 15 wenye umri wa miaka 15 hadi 19 amejifungua, na pia kuwa mimba milioni 1.1 n... Continue reading ->


Source: Kwanza TVRead More