utalii wa Tanzania wafikishwa Korea - Kwanza TV | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

utalii wa Tanzania wafikishwa Korea

MWENYEKITI wa Utalii Tanzania (TTB), Jaji Thomas Mihayo na Mkurugenzi Mwendeshaji wa bodi hiyo, Devota Mdachi, wamekutana na wadau mbalimbali wa sekta ya utalii jijini Seoul, Korea ya Kusini kwa ajili ya kutangaza utalii wa Tanzania.


Mikutano hiyo, iliandaliwa kwa kushirikiana na ofisi ya Ubalozi wa Tanzania nchini humo, imeanza kufanyika Julai 4 hadi 8, mwaka huu ili kuendeleza mikakati ya kukamata soko la utalii kwa mashariki ya mbali.


Akizungumzia mkutano huo, Jaji Mihayo alisema ziara hiyo imekuwa ya mafanikio makubwa kutokana na mwitikio mzuri waliopata kutoka kwa wadau wa utalii waliokutana nao.


Alisema ujumbe kutoka TTB, ulifanikiwa kukutana na wadau mbalimbali wakuu wa utalii wa nchi hiyo akiwemo Byeong -Sam Kim ambaye ni Katibu Mkuu wa Chama cha Mawakala wa Utalii wa Korea Ya Kusini (Korean Tourism Assistance).


Katika kikao hicho, TTB na KTA waliweza kufanya mazungumzo yaliyolenga kuhamasisha suala la ushirikiano baina ya mawakala wa utalii wa Tanzania na Korea ya Kusini.


Nay... Continue reading ->


Source: Kwanza TVRead More