UTURUKI YAAMUA KUKUNUA MFUMO WA KUJILINDA URUSI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

UTURUKI YAAMUA KUKUNUA MFUMO WA KUJILINDA URUSI

Na Ripota Wetu
WAZIRI wa Ulinzi nchini Uturuki Hulusi Akar amesema nchi yake inajiandaa kwa vikwazo vya Marekani baada ya kuendelea na mpango wake wa kununua mfumo wa kujilinda na makombora kutoka Urusi.
Katika taarifa iliyosambazwa jana Jumatano, Akar amesema wametuma watu wake nchini Urusi kupewa mafunzo ya kutumia mfumo huo wa S-400, yatakayoanza siku chache zijazo na kuendelea kwa miezi kadhaa.
Inadaiwa kuwa Ikulu ya White House ilitishia kuiwekea vikwazo Uturuki, chini ya sheria ya vikwazo inayozuia shughuli za kibiashara na sekta ya intelijensia na ulinzi ya Urusi.
Hata hivyo Marekani, inataraji kuiongezea mbinyo Uturuki, ambayo ni mshirika wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO ili kununua mfumo wa Marekani, lakini Uturuki imekataa kuachana na ununuzi wa mfumo huo wa Urusi.
CHANZO -DW SWAHILI... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More