Uwoya Afungukia Mahusiano Yake na Diamond - Ghafla TZ | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Uwoya Afungukia Mahusiano Yake na Diamond

Muigizaji wa Bongo movie Irene Uwoya amefunguka na kuelezea Mahusiano Yake na staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz baada ya kuzua gumzo siku za hivi karibuni.


Uwoya na Diamond walitengeneza headlines mwishoni  wa wiki iliyopita baada ya Diamond kumposti Mrembo huyo Kwenye ukurasa wake wa Instagram bila kuweka caption yoyote jambo lililozua maswali mengi.


Pamoja na maneno ya hapa na pale ilikuja kujulikana kama Diamond alikuwa amemlipa Uwoya kwa ajili ya ku host Shindano la Jibebe challenge ambalo lilifanyika siku ya Jumapili.


Pamoja na hayo bado Kumekuwa na tetesi kuwa Wawili hao wana mahusiano ya zaidi ya kikazi ilihali Uwoya ni Mke wa Msanii wa Bongo fleva Dogo Janja.


Kwenye mahojiano na SnS Tanzania (Simulizi na Sauti) Uwoya amesema kuwa alichukulia kitendo Cha Diamond kumposti  kawaida ingawa watu walitafsiri vibaya lakini hana Mahusiano na Msanii huyo zaidi ya urafiki wa kawaida:Sioni kama ni tatizo kwa sababu aliposti tu picha ambayo mtu mwingine anaweza akaposti. Watanzania wanapenda tu kufikiria vitu, ku-judge wanavyoweza wao, haikuwa tatizo kwangu”.Siku ya Jumapili Kwenye Biko Jibebe Challenge  Irene Uwoya ndiye alikuwa host wa tukio hilo. Shindano hilo lilianzishwa na Diamond baada ya kutoa wimbo wake unaokwenda kwa jina la Jibebe ambao ameshirikiana na Mbosso na Lava Lava.


The post Uwoya Afungukia Mahusiano Yake na Diamond appeared first on Ghafla!Tanzania.


Source: Ghafla TZRead More