UWT TEMEKE WAMPONGEZA RAIS MAGUFULI KWA KUNUNUA NDEGE YA NNE BOEING 787-8 DREAMLINER - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

UWT TEMEKE WAMPONGEZA RAIS MAGUFULI KWA KUNUNUA NDEGE YA NNE BOEING 787-8 DREAMLINER

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.JUMUIYA ya Umoja  wa Wanawake  Tanzania (UWT) Wilaya ya Temeke wamempongeza Mwenyekiti wa Chama hicho na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufulu kwa kuweza kutekeleza ahadi ya kununua ndege ya nne kati ya saba alizoziahidi.
UWT Temeke wamesema kuwa hiyo ni moja ya ahadi zilizoanishwa katika Ilani ya Chama cha Mapinduzi na wamemuomba aweze kutimiza ahadi zote ili kuhakikisha upinzani wanakosa la kusema.
Akizungumza na wajumbe wa UWT Wilaya ya Temeke, Mgeni rasmi Mbunge wa Viti Maalum  Mkoa wa Dar es Salaam Mariam Kisangi  amesema kuwa serikali ya awamu ya tano ya Chama cha Mapinduzi imedhamiria kutimiza ahadi zote zilizoanishwa wakati wa kampeni  na tayari zinafanyiwa kazi ikiwemo kununua ndege ya nne kati ya saba na zile zitakazoanza kutekelezwa kwenye bajeti ya 2018/19.
"Rais wetu Dkt Magufuli aliahidi kununua ndege saba zitakazokuwa mali yetu na mpaka sasa ameshanunua ndege  ikiwemo Boeing  787-8 Dreamliner  na kutimiza idad... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More