UZALISHAJI WA SUKARI WAONGEZEKA TPC - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

UZALISHAJI WA SUKARI WAONGEZEKA TPC

Na Vero Ignatus, Kilimanjaro.Kiwanda cha Sukari TPC kimeongeza uzalishaji wa sukari kutoka tani 36,000 ambayo ilikua ikizalishwa mwanzoni kabla ya ubinafsishaji na kufikia tani 110,000 ikiwa ni juhudi za kutatua changamoto ya upungufu wa sukari ya majumbani nchini ambayo ni tani 100,005.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Utawala kiwanda cha TPC ,Jaffari Ally alisema hayo katika ziara ya Naibu Waziri wa Kilimo Omari Mgumba pamoja na Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Joseph Kakunda katika kiwanda hicho ambapo alisema kuwa bado wanaendelea na upanuzi wa mashamba na wanatarajia kuzalisha tani 120,000 .
Jaffari aliipongeza serikali kwa kuziba mianya ya biashara magendo ya sukari ambapo sukari zisizokidhi viwango zilizua zikiingizwa nchini na kushindanishwa katika masoko ya ndani hivyo kuathiri viwanda vya ndani.
“Wazalishaji wa sukari tunapenda kuipongeza serikali ya awamu ya tano kwa kuzibiti mianya ya uingizwaji holela wa sukari ,miaka ya nyuma soko lilichafuliwa na sukari iliyokua ikiingizw... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More