UZINDUZI WA ALBAM YA MAMA WA HIYARI YA AMIGO KUNOGESHWA NA WAKONGWE WA TAARAB - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

UZINDUZI WA ALBAM YA MAMA WA HIYARI YA AMIGO KUNOGESHWA NA WAKONGWE WA TAARAB

Na.Khadija Seif,Globu ya jamii.
Kundi la taarab First class modern taarab linalofanya vizuri kwa sasa linatarajia kufanya uzinduzi wa albam yao ya kwanza tarehe 10 mwezi huu jijini Dar es salaam.
Akizungumza na wadau pamoja na wanahabari Jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa bendi hiyo Aboubakar Soud maarufu kama Prince Amigo amesema kuwa bendi hiyo ilianzishwa rasmi mwaka huu na kuiona fursa ya kutoa burudani yenye hadhi na heshima kwa rika zote. 
Aidha amefafanua ujio wa First Class Modern Taarab ambao umekusanya vijana wengine kutoka bendi kongwe hapa nchini lengo likiwa ni kutoa uhondo wa hadhi.Amigo ameeleza kuwa albam hiyo itazinduliwa rasmi katika ukumbi wa travertine Magomeni na kusindikizwa na wakongwe wa taarab nchini kama sabaha Salum muchacho, Rukia Ramadhani ,Mwanahawa Ally, Mwanamtama Amir pamoja na Patricia Hillary.
Msemaji wa bendi hiyo kwa upande wa matayarisho Haji Mabovu ameeleza kuwa tiketi zinapatikana kwa bei ya kitanzania shilingi elfu tano na getini zinapatikana kwa b... Continue reading ->Source: Issa MichuziRead More