Uzinduzi wa chupa mpya ya K-vant - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Uzinduzi wa chupa mpya ya K-vant

Kampuni ya Mega Beverages Company Limited,ya mkoani Arusha, inayotengeneza pombe kali chapa maarufu ya K-Vant, imezindua chupa mpya za kinywaji cha K-Vant zenye mwonekano tofauti na wakisasa. Uzinduzi huu wa jijini Arusha unafuata baada ya uzinduzi mkubwa ulio fanyika jijini Dar es Salaaam wiki moja iliyopita.Mabadiliko hayo hayatabadirisha ladha halisi ya kinywaji hicho na wateja wake wataendelea kuifurahia ikiwa katika ladha yake halisi ya siku zote.


Lengo kubwa la kubadilisha mwonekano wa chupa za pombe ya K-Vant, ni mkakati wa kampuni wa kukuza masoko yake ya ndani na nje ambapo imelenga kuwa katika mwonekano bora zaidi bila kuathiri ladha halisi ya kinywaji hicho.


Hafla ya uzinduzi huo ilifanyika katika hoteli ya Mount Meru jijini Arusha. Katika sherehe hiyo pia, Meneja Masoko na Mauzo wa Mega Beverages Company Limited, Marco Maduhu alisema, “Kampeni mpya ya kinywaji cha K-Vant katika mwonekano mpya ni ’Ni Halali Yako’ kampuni imejikita katika kuimarisha usambazaji wa bidhaa ya pombe ya K-Vant katika sehemu zote nchini ili watanzania waendelee kufurahia ubora wake ikiwa katika mwonekano wa chupa mpya na katika ladha ile ile waliyoizoea siku zote,”.


The post Uzinduzi wa chupa mpya ya K-vant appeared first on Bongo5.com.


Source: Bongo5Read More