VAN GAAL ATANGAZA RASMI KUSTAAFU UKOCHA NA KUACHANA NA SOKA - Mwanaharakati Mzalendo | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

VAN GAAL ATANGAZA RASMI KUSTAAFU UKOCHA NA KUACHANA NA SOKAAliyewahi kuwa kocha wa Manchester United, Lous Van Gaal ametangaza kustaafu kufundisha mpira akiwa na umri wa miaka 65.
Kocha huyo raia wa Uholanzi, aliacha kuifundisha Man U mwaka 2016 ambapo alitamka mbele ya waandishi wa habari kwamba hiyo ndio itakuwa timu yake ya mwisho kuifundisha.
“Mimi ni mstaafu sasa. Sina shauku ya kutaka kuwa mkurugenzi wa ufundi wala mchambuzi wa soka kwenye TV,” Van Gaal aliiambia show ya Dutch TV iitwayo VTBL. 
“Mke wangu Truus aliacha kazi yake miaka 22 iliyopita kwa ajili yangu na alinifuata kila nilipokuwa naenda nchi nyingine. Nilimuahidi kuwa nitastaafu nifikapo miaka 55 lakini sikufanya hivyo mpaka sasa nina miaka 65. 
“Ana haki ya kuwa na maisha na mimi nje ya mpira wa miguu. Naweza kusema ana furaha sana. Nadhani ningeweza kufanya kazi kama mkurugenzi wa ufundi. 
Van Gaal amefundisha timu zifuatazo:
Ajax (1991-1997), FC Barcelona (1997-2000 na 2002-2003), Netherland (2000-2001/2012-2014), Holland Sub20 (2001), AZ Alkmaar (2005-2009), Bayern... Continue reading ->
Source: Mwanaharakati MzalendoRead More