VETA Kihonda yatoa mafunzo kwa madereva wa magari makubwa zaidi ya 1500 - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

VETA Kihonda yatoa mafunzo kwa madereva wa magari makubwa zaidi ya 1500

Chuo cha VETA Kihonda kimetoa mafunzo kwa madereva wa magari makubwa  zaidi ya 1500 kwa kipindi cha kuanzia mwezi Januari mwaka huu lengo likiwa ni kupunguza ajali ambazo zinatokana na makosa ya kibinadamu.
Chuo cha VETA Kihonda  ni  Chuo ambacho kimebobea katika utoaji wa mafunzo ya udereva magari makubwa ambapo madereva wa magari makubwa wanatakiwa kupata mafunzo hayo hapo au vyuo vingine vilivyosajiliwa vikiwa na mafunzo hayo.
Mwalimu wa Udereva wa Magari Makubwa na Mabasi wa chuo cha VETA Kihonda William Munuo amesema kuwa madereva wengi wanajua kuendesha kwa kunyoosha katika barabara lakini kurudi nyuma ni tatizo ambapo wengi ndio wanasababisha ajali au kuangusha magari hayo na kuleta hasara kwa makampuni.
Munuo amesema mafunzo waliyoyaanza ni endelevu na kutaka madereva kuzingatia mafunzo hayo na kuyaishi katika kuendesha na hatimaye watakuwa madereva bora.
Munuo amesema mafunzo hayo yanafanya magari makubwa kuishi muda mrefu kutokana  na wakati mwingine yanapata ubovu kwa uendes... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More