Victor Wanyama atoa ahadi ya Signed Boot katika Ndondo Cup 2018 - Shaffih Dauda | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Victor Wanyama atoa ahadi ya Signed Boot katika Ndondo Cup 2018

Mchezo wa kwanza wa michuano ya Ndondo Cup kwa mwaka 2018 umepigwa leo kwa mchezo kati ya wauza Ferniture wa Keko dhidi ya Mabibo Market mchezo ulioisha kwa Mabibo Market kuibuka kidedea kwa mabao 3-2.


Watu wengi maarufu walikuwepo katika mchezo huu wa leo na moja kati ya watu maarufu waliokuwepo alikuwa ni nyota wa Tottenham Hotspur Victor Wanyama ambaye aliambatana na marafiki zake kutoka Kenya.


ShaffihDauda.co.tz na Dauda Tv tulifanikiwa kufanya mahojiano na Wanyama ambapo pamoja na kumwaga sifa kwa mwenyekiti wa michuano hii Shaffih Dauda lakini pia Wanyama alisema upo uwezekano wa kutoa kiatu kwa mfungaji bora wa ambacho kinaweza kuwa na saini yake.


Akijibu swali la mtangazaji wa Dauda Tv kuhusu kutegemea chochote kutoka kwake, Wanyama alisema “tutarajie chochote kinaweza kufanyika, ninaweza kutoa signed boot ama lolote lile tutarajie'”, full video ya mahojiano kati ya Dauda Tv na Wanyama hii hapa tumekuwekea.


... Continue reading ->Source: Shaffih DaudaRead More