Video: Kosa la kumruhusu nyani kuendesha basi la abiria lamfukuzisha kazi dereva - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Video: Kosa la kumruhusu nyani kuendesha basi la abiria lamfukuzisha kazi dereva

Aliyekuwa dereva wa basi la abiria nchini India, M. Prakash amefukuzwa kazi mwishoni mwa juma hili baada ya kukutwa na kosa la kumruhusu nyani kuendesha basi la abiria ambalo yeye alikuwa akiliendesha.
M. Prakash mwenye umri wa miaka 36 amekutwa na kosa hilo baada ya video ya tukio hilo kusambaa kwenye mitandao ya kijamii.


Dereva huyo amefanya tukio hilo Oktoba 1 ya mwaka huu wakati basi hilo likiwa katika safarini zake za kawaida kutoka Davangere na kuelekea Halekall huko nchini India.Msemaji wa Shirikisho la usafiri wa barabara hiyo ya Karnataka (KSRTC), T.S. Latha ameiyambia IANS kuwa licha ya abiria kutolalamika kitendo hicho ila hawawezi kuacha maisha yao kuwa hatarini kwa kosa la dereva kumruhusu nyani kuwa kwenye msukani.The post Video: Kosa la kumruhusu nyani kuendesha basi la abiria lamfukuzisha kazi dereva appeared first on Bongo5.com.... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More