Video-Miaka 20 ya George Kavila kwenye ligi anahitaji nini kama si heshima? - Shaffih Dauda | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Video-Miaka 20 ya George Kavila kwenye ligi anahitaji nini kama si heshima?

Vuta picha mwaka 1998 ulikuwa na umri gani, ukikuwa wapi na ulikuwa unafanya nini?


Tangu wakati huo ni miaka 20 sasa imepita, mambo mengi mazuri na mabaya yamepita kama mtoto alizaliwa mwaka huo kwa sasa ni kijana ambaye kwa mujibu wa sheria za Tanzania anaruhusiwa kuoa na kuolewa.Mabibi na Mabwana namleta kwenu moja ya ma-legendary wa VPL George Kavila ambaye ameitumikia ligi ya Tanzania bara tangu 1998 (miaka 20 sasa). Kwa kifupi ameanza kucheza ligi kuu kabla ya Kabwili, Mkomola, Kibabage, na wengine wengi hawajazaliwa hadi leo bado anatwanga nao.Katika miaka 20 aliyocheza ligi ya Tanzania amedumu Kagera Sugar kwa miaka 10 (ambako yupo hadi sasa) na miaka 10 mingine imegawanyika katika vilabu mbalimbali.


Kavila amekutana na mikasa mingi ambayo unatakiwa kuifahamu, kwakuwa mimi ni jukumu langu kukupa mikasa hiyo nimemtafuta Kavila na amesimulia kila kitu mwanzo mwisho.


Wachezaji wengi wa timu ambazo hazina majina makubwa wanaogopa kucheza mechi dhidi ya Simba na Yanga, Kavila ana... Continue reading ->


Source: Shaffih DaudaRead More