Video: Msanii wa Uingereza Big Shaq alivyokusanya kijiji Elements Dar - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Video: Msanii wa Uingereza Big Shaq alivyokusanya kijiji Elements Dar

Mashabiki wa muziki nchini Tanzania weekend hii walipokea show ya nguvu katika kiota cha burudani cha Elements kutoka kwa msanii wa muziki kutoka nchini Uingereza, Michael Dapaah aka Big Shaq show ambayo ilidhaminiwa na kinywaji cha, Budweiser.


Mastaa wa muziki ambao walihudhia show hiyo ni pamoja na rapa Lord Eyes kutoka Arusha, Mtangazaji wa The Playlist ya Times FM Lil Ommy, Idris Sultan, T-Bway, Moko Biashara pamoja na Quick Rocka ambaye ni balozi wa kinywaji hicho pamoja na wadau wengine wengi.


Show hiyo ilianza majira ya saa 7 usiku ambapo rapa huyo aliingia ukumbini na kupanda kwenye steji kwa ulinzi mkali huku shangwe zikipigwa na mashabiki wengi waliofurika ukumbini hapo.

DJ Sinyorita akisababisha mambo


Rapa huyo alianza show yake na wimbo Man Don’t Dance ambao ulipolewa kwa shangwe kubwa. Shaq alifanya show hiyo kwa dakika 20 na alifunga show yake hiyo na wimbo, Mans Not Hot ambao uliwafanya mashabiki arudie mara mbili.Mashabiki wakila burudani


The post Video: Msanii wa Uin... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More