Video: Nyumba 32 za bomolewa Dar, wananchi walala nje, wadai waliingizwa mkenge na kiongozi wa Mtaa - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Video: Nyumba 32 za bomolewa Dar, wananchi walala nje, wadai waliingizwa mkenge na kiongozi wa Mtaa

Wananchi wa Kitongoji cha Yangeyange Kata ya Msongola Ilala jijini Dar es salaam wamejikuta wakiwa katika wakati mgumu baada ya nyumba zao zaidi ya 32 kubomolewa na kampuni moja ya udalali iitwayo, Lumina kwa madai kwamba wamepewa oda hiyo na Mahakama baada ya mteja wao ambaye anajulikana na kwa jina moja, Scolastica kushinda kesi ya uvamizi katika viwanja hicho.







Tukio hilo limetokea tarehe 9 Machi 2019 na mpaka sasa Wananchi hao pamoja na watoto wao wanalala nje chini ya miti katika eneo.





Wananchi hao wanadai kwamba hawakuwa na taarifa ya kwamba viwanja nyao vipo kwenye migogoro na kesi ipo Makahamani mpaka walivyokuja watu hao na kuanza kubomoa.





Akiongea na mwandishi wetu, mmoja kati ya wahanga wa tukio hilo aitwaye, Pendo Masanja alidai yeye alinunua eneo hilo toka mwaka 2016 chini ya viongozi wa serikali ya Mtaa na alianza kujenga tararibu mpaka alivyomaliza na kuhamia na familia yake.





“Sikuwahi kusikia kwamba eneo hili lina mgogoro toka nimekuja hapa, nimeanza ku... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More