VIDEO: Vita ya Juventus vs Man United, Real Madrid kazi ipo! - Mwanaspoti | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

VIDEO: Vita ya Juventus vs Man United, Real Madrid kazi ipo!

MICHUANO ya ligi ya Mabingwa ulaya inaendelea tena leo. Baada ya jana usiku kushuhudia miamba kadhaa ya soka ikitandikwa bila huruma, leo macho na masikio, yanaelekezwa katika viwanja nane tofauti barani Ulaya.
Kwa wale wasiokuwa na matokeo ni kwamba, usiku wa Jana, Monaco ya Thiery Henry, ilitandikwa 0-4 na Club Brugge, Atletico Madrid ikaitandika Borrusia Dortmund 2-0, Barcelona na Inter zikatoka sare ya 1-1.
Tottenham Hotspur, ikailaza PSV Eindhoven 2-1, Liverpool ikalimwa 1-2 na FK Crvena Zvezda, Napoli na PSG zikatoshana nguvu (1-1), FC Porto ikaitandika Lokomotiv Moscow 4-1 huku Schalke 04 wakiilamba Galatasaray 2-0.
Leo Usiku, FC Bayern Munchen itaumana na AEK Athens, Benfica v Ajax, Lyon v Hoffenheim, Manchester City wakiikaribisha Shakhtar Donetsk pale Etihad, CSKA Moscow v Roma, Viktoria Plzen v Real Madrid, Valencia v Young Boys na Juventus itailika Manchester United, nchini Italia.
Kuelekea mechi hizo sasa, Mwanaspoti Digital, inakuchambulia hatua kwa hatua mechi zote hizo ... Continue reading ->


Source: MwanaspotiRead More