Vifo vya Wajawazito vimepungua kwa asilimia 40-Waziri Ummy Mwalimu - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Vifo vya Wajawazito vimepungua kwa asilimia 40-Waziri Ummy Mwalimu

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
Serikali imesema kuwa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali katika Sekta  ya afya wameweza kupunguza vifo vya wamama wajawazito kwa asilimia 40.
Hayo ameyasema Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati akifungua jengo la Huduma za Afya Binafsi katika Hospitali ya CCBRT, amesema kuwa vifo vya akina mama vilikuwa vingi kutokana na kukosekana kwa baadhi ya huduma lakini sasa Serikali imejenga vituo vya Afya 350 ikiwa pamoja na kuweka huduma za dharula ya kumtoa mtoto tumboni.
Amesema kuwa CCBRT imekuwa ni moja ya Hospitali iliyoweza kupambana na ugonjwa wa Fistula ambao ilikuwa unafanya wanawake kukosa amani. Mwalimu amesema serikali imeondoa kodi katika dawa, vifaa tiba pamoja na vitendanishi ikiwa ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na kwa gharama nafuu. Aidha ameiagiza Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kulipa kwa wakati madai ya watoa huduma za afya ili fedha hizo ziweze kuendesha huduma mbalimbali ikiwe... Continue reading ->Source: Issa MichuziRead More