VIJANA NCHINI WAASWA KUANZISHA MIRADI YA KIMKAKATI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

VIJANA NCHINI WAASWA KUANZISHA MIRADI YA KIMKAKATI

Vijana nchini watakiwa kubadili mtazamo kwa kuanzisha miradi ya kimkakati itakayowawezesha kiuchumi.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (Mb) alipofanya ziara hiyo Mkoa wa Iringa kwa lengo la Kuhamasisha na kukagua maeneo ya ujenzi wa Vitalu Nyumba (Green House) na uwepo wa miundombinu itakayotumika kwenye maeneo hayo.
Mheshimiwa Mhagama amesema sekta ya kilimo inaajiri na kuchangia katika pato la taifa kwa zaidi ya asilimia 60%, hivyo vijana ambao ndio nguvu kazi ya taifa wakatumie rasilimali ardhi kama mtaji wa kujiajiri na kuweza kuajiri wenzao.
“Lengo letu ni vijana kutumia sekta hii ya umahiri kwa ajili ya kuwaondoa kwenye mitazamo finyu na kuwa na mitazamo chanya ili waweze kunufaika na miradi itakayo buniwa na kutumika kama mfano kwa vijana nchi nzima.” Alisema Waziri Mhagama
Aliongeza kuwa vijana watafundishwa kilimo cha Kitalu nyumba ambavyo vitawawezesha kuongeza thamani kwenye mazao... Continue reading ->
Source: Issa MichuziRead More