VIJANA WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA - Kajunason | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

VIJANA WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA

Vijana wa Kata ya Kunduchi wametakiwa kujitokeza kwa wingi kwenda kuchukua mikopo iliyotengwa na halmashauri, kwani ni haki yao ya msingi na ni agizo kwa kila halmashauri kuweza kutenga asilimia nne kwa vijana, asilimia nne kwa wakina mama na asilimia mbili kwa ajili ya walemavu.
Rai hiyo imetolewa jana eneo la Kunduchi jijini Dar es salaam na Katibu wa Idara ya Hamasa na Chipukizi wa UVCCM Taifa Bw. Hassan Bomboko alipokuwa mgeni rasmi katika Bonanza la Vijana lililoandaliwa na UVCCM kata ya Kunduchi.Katibu wa Idara ya Hamasa na Chipukizi wa UVCCM Taifa Bw. Hassan Bomboko Akiongea na vijana wa kata ya Kunduchi mapema jana jijini Dar es salaam.Vijana wa UVCCM kata ya Kunduchi wakicheza singeli katika bonanza la vijana wa kata hiyo mapema jana.
Katibu huyo alisema kuwa amesikitishwa sana kusikia vijana wanaziogopa fedha hizo zinazotokana na pato la Halmashauri, na kusababisha kupelekwa katika makundi mengine kama UWT, na kutoa maelekezo kwa Mwenyekiti wa Vijana wa kata hiyo kuhakikisha vi... Continue reading ->


Source: KajunasonRead More