VIJANA WATAKIWA KUWA WABUNIFU KATIKA BIDHAA ZAO ILI KUKIDHI USHINDANI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

VIJANA WATAKIWA KUWA WABUNIFU KATIKA BIDHAA ZAO ILI KUKIDHI USHINDANI

Na. Vero Ignatus,Arusha


Vijana nchini Tanzania wametakiwa kuwa wabunifu kwa kubuni bidhaa zinazoweza kuhimili ushindani katika soko la pamoja la Afrika Mashariki ili waweze kunufaika na fursa za uwepo wa soko hilo pamoja na kuboresha maisha yao.


Hayo yanesemwa na Wawakilishi wa vijana kutoka Majukwaa ya vijana Wilaya ya Arusha katika Mafunzo ya Ujasiriamali yanayolenga kukuza ubunifu na uwezo wa vijana kutumia fursa za kimasoko kujikwamua kiuchumi .

Farida Charles na Denis George walisema kuwa ,vijana wengi wamekuwa wakijitahidi kubuni bidhaa zao lakini changamoto kubwa bado ipo katika ubora wa hizo bidhaa katika kushindana na soko la Afrika Mashariki.

Kutokana na changamoto hiyo vijana hao kwa pamoja walijiwekea mikakati ya kuhakikisha kuwa bidhaa zote wanazozalisha ni lazima ziendane na soko la Eac ili kuweza kunufaika na fursa mbalimbali zilizopo na kupata masoko zaidi.

Mratibu wa shirika la Vijana la Initiative for Youth ,Laurent Sabuni alisema kuwa, vijana wa k... Continue reading ->
Source: Issa MichuziRead More