VIKUNDI VYA UPATU KUTOSIMAMIWA NA SHERIA MPYA HUDUMA NDOGO ZA FEDHA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

VIKUNDI VYA UPATU KUTOSIMAMIWA NA SHERIA MPYA HUDUMA NDOGO ZA FEDHA

Na Farida Ramadhani, WFM, Dodoma
Serikali imesema kuwa vikundi vya Upatu havitasimamiwa chini ya Sheria mpya ya Huduma Ndogo za Fedha ya Mwaka 2018 (The Microfinance Act, 2018)kwa sababu havijihusishi na biashara ya huduma ndogo za fedha.
Hayo yameelezwa bungeni jijini Dodoma na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) wakati akihitimisha hoja za mjadala waMuswada wa Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha ya Mwaka 2018.
Dkt. Mpango alisema Sheria hiyo itahusisha taasisi kama vile Vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo (SACCOS), Taassi za huduma ndogo za fedha zisizopokea na zinazopokea amana na vikundi vya kifedha vya kijamii, wakopeshaji binafsi na asasi za kijamii.
Alieleza kuwa Sheria hiyo pia inalenga kuwalinda wananchi wanaotegemea sekta ndogo ya fedha katika kuendesha maisha yao na shughuli za kiuchumi kwa ujumla na itasimamia na kudhibiti biashara ya huduma ndogo za fedha, kuwawezesha watumiaji na watoa huduma hiyo pamoja na kudhibiti changamoto zinazoweza kutokea kati... Continue reading ->Source: Issa MichuziRead More