VILABU SITA UINGEREZA VYASAKA SAINI YA MSHAMBULIAJI MBWANA ALLY SAMATA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

VILABU SITA UINGEREZA VYASAKA SAINI YA MSHAMBULIAJI MBWANA ALLY SAMATA

MSHAMBULIAJI nyota katika Ligi ya Ubelgiji anayekipiga Klabu ya Genk na nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Mbwana Samatta huenda akatua Ligi Kuu ya England (EPL) msimu ujao.
Samatta anayejulikana zaidi kwa jina Samagoal, amedokeza hadi sasa kuna vilabu sita vya Ligi ya Primia ambavyo vinapigana vikumbo kumsajili nyota huyo ambapo mwenyewe amenukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari akieleza kuwa hayupo katika wakati mzuri kusema klabu gani anaweza kwenda.
Mchezaji huyo amefafanua kutoka Hispania kuna timu mbili ambazo zimekuwa zikiisaka saini yake lakini ndoto yake kubwa ni kucheza katika Ligi Kuu ya England. Hata hivyo inaelezwa si mara ya kwanza kwa mchezaji huyo kudaiwa kuwindwa na vilabu vya Ligi ya Premia. CHANZO -BBC ... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More