VIONGOZI TFF WAACHE UBISHI, SIMBA NA YANGA ICHEZESHWE NA MAREFA WA KIGENI TU - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

VIONGOZI TFF WAACHE UBISHI, SIMBA NA YANGA ICHEZESHWE NA MAREFA WA KIGENI TU

KLABU ya Yanga SC imeandika barua Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kulalamika vitendo visivyo vya kiungwana walivyofanyiwa wachezaji wao na wachezaji wa mahasimu wao, Simba SC Jumapili iliyopita, Septemba 30 katika pambano la Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
Msemaji wa Yanga SC, Dissmas Ten aliwaambia Waandishi wa Habari mwanzoni mwa wiki hii mjini Dar es Salaam kwamba wamelazimika kuyaripoti TFF baadhi ya matukio yaliyofanyika katika mchezo huo ili hatua zichukuliwe, akitolea mfano kitendo cha kiungo Mghana wa Simba SC, James Kotei kumpiga ngumi beki wao, Gardiel Michael na refa Jeonesiya Rukyaa wa Kagera hakuchukua hatua.

“Kwenye mchezo uliopita kuna matukio ambayo si ya kiungwana yalitokea uwanjani, sisi kama klabu tumeandika barua kwenda TFF na bodi ya Ligi kuomba mamlaka hizo kuchukua hatua stahiki kwa matukio yote yasiyo ya kiungwana yaliyotokea,” amesema Ten na kuongeza.
“Huwezi kusema sana kulingana na mchezaji aliyefanya hayo matukio, mfano mc... Continue reading ->
Source: Bin ZuberyRead More