VIONGOZI WA KISIASA TUHAMASISHE WANANCHI KUENZI UTAMADUNI WAO - WAZIRI MKUU - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

VIONGOZI WA KISIASA TUHAMASISHE WANANCHI KUENZI UTAMADUNI WAO - WAZIRI MKUU

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wanasiasa wakiwemo mawaziri na wabunge wawahamishe Watanzania kuendeleza utamaduni wao.
Ametoa wito huo leo (Jumatano, Julai 18, 2018) wakati akizungumza na wazee na wananchi wa Makunduchi mara baada ya kushuhudia maadhimisho ya sikukuu ya Mwaka-Kogwa yaliyofanyika Makunduchi, wilaya ya Kusini, mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar.
“Mawaziri wote, tuna dhamana ya kuwahamasisha Watanzania waendeleze utamaduni ili uwe ni jambo hai. Wabunge na wawakilishi tukiwa kwenye majukwaa, tusisitize Watanzania waendeleze utamaduni,” amesema.
Amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) pamoja na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) zinasimamia uwepo wa utamaduni na zenyewe zinaongozwa na Ilani ya Chama cha Mapinduzi ambayo imelenga kuihamasisha  jamii kuuenzi,  kuulinda  na  kuudumisha utamaduni wa Mzanzibari na kushiriki katika uandaaji wa matamasha 50 ya utamaduni.
“Lazima utamaduni uendelezwe ndani na nje ya nchi na ni lazima tufanye jitihada t... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More