VIONGOZI WA NGAZI MBALIMBALI NA WANANCHI WASHIRIKI KATIKA MAZISHI YA BABA YAKE MZAZI MAMA SALMA KIKWETE - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

VIONGOZI WA NGAZI MBALIMBALI NA WANANCHI WASHIRIKI KATIKA MAZISHI YA BABA YAKE MZAZI MAMA SALMA KIKWETE

Na Hadija Seif, Globu ya Jamii
VIONGOZI wa ngazi mbalimbali Serikalini , viongozi wastaafu pamoja na mamia ya wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam wameshiriki katika mazishi ya mzee Rashid Mkwachu ambaye ni baba yake mzazi Mke wa Rais mstafu Jakaya Kikwete, Mama Salma Kikwete.

Mwili wa mzee Mkwachu umezikwa leo katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam. Alifikwa na umauti Julai 19 mwaka huu  na chanzo cha kifo chake kimeelezwa na Msemaji wa familia ya Kikwete Ridhawani Kikwete kuwa mzee huyo amefariki kutokana na magonjwa ya utu uzima kwani umri wake ulikuwa zaidi ya miaka 100.

Kabla ya mwili kufikishwa makaburi ya Kisuti ibada na dua kumuombea marehemu mzee Mkwachu zilifanyika nyumbani kwa Rais mstaafu Jakaya Kikwete Msasani jijini Dar es Salaam. Baadhi ya viongozi walioshiriki kwenye maziko hayo ni Rais Mstaafu Al haji Ali Hassan Mwinyi,  Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa.

Akizungumza kwenye msiba huo Mufti wa... Continue reading ->







Source: Issa MichuziRead More