“VITENDO VYA UKEKETAJI KWA WATOTO WADOGO NCHINI VICHUNGUZWE”- DKT. NDUGULILE. - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

“VITENDO VYA UKEKETAJI KWA WATOTO WADOGO NCHINI VICHUNGUZWE”- DKT. NDUGULILE.

Na Mwandishi Wetu Dar es Salaam.Serikali imeagiza kuchunguzwa kwa vitendo vya ukatili hasa ukeketaji kwa watoto wachanga unaondelea kufanyika nchini kwa baadhi ya makabila yenye mila za ukeketaji wamebadili mbinu na kuanza kukeketa watoto wachanga kwa lengo la kukwepa mkono wa sheria.
Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile leo wakati akiongea na vyombo vya habari katika mdahalo wa wahariri wa vyombo vya habari kuhusiana masuala ya ukeketaji,mimba na ndoa za utotoni.
Naibu Waziri Ndugulile amesema kufuatia jamii hizo kubadili mwenendo wa ukeketaji na Serikali kubaini mbinu hizo amesisitiza agizo lake alilolitoa wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike yaliyofanyika Mkoani Arusha la kuwataka madaktari wote nchini kufanya uchunguzi kwa watoto wote wachanga ili kubaini kama watoto hao wamefanyiwa ukatili kwa kukeketwa ili wahusika wafikishwe kwenye vyombo vya sheria.
Dkt. Ndugulile aliongeza kuwa utafi... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More