Viwanja Afrika machinjio ya mashabiki - Shaffih Dauda | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Viwanja Afrika machinjio ya mashabiki

Mtu mmoja amefariki dunia na wengine 40 kujeruhiwa kwenye vurugu zilizotokea kabla ya mchezo wa kufuzu AFCON kati ya Madagascar na Senegal huko Antananarivo siku ya Jumapili.


Vurugu hizo zilitokana na idadi kubwa ya watazamaji kutaka kuingia uwanjani kwenye uwanja mdogo  unaoingiza watu 22,000 huku maelfu wakikosa nafasi ya kuingia.


Matukio ya vifo uwanjani vinavyotokana na vurugu vimekuwa maarufu barani Afrika ambapo moja ya tukio baya lilitokea Accra Sports Stadium ambapo mashabiki 127 walifariki mwaka 2001 baada ya polisi kupiga bomu la machozi kwenye mapambano baina ya Hearts of Oak na Asante Kotoko.


Mwaka 2012 mashabiki 74 nchini Misri walifariki kwenye mchezo kati ya Al Masry na Al Ahly kwenye dimba la Port Said.


Mwakajana mashabiki nane walifariki dunia nchini Malawi na idadi hiyohiyo ya vifo ilitokea kwenyw fainali nchini Senegal. Pia mashabiki wawili walifariki mwezi July mwaka jana nchini Afrika Kusini kwenye mchezo wa Soweto derby baina ya Kaizer Chiefs dhidi ya Orlando Pir... Continue reading ->


Source: Shaffih DaudaRead More