VYAMA 14 VYAJITOKEZA KUGOMBEA UDIWANI, UBUNGE - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

VYAMA 14 VYAJITOKEZA KUGOMBEA UDIWANI, UBUNGE

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema kuwa jumla ya wagombea 13  walichukua fomu za kuomba kuteuliwa kugombea nafasi ya Ubunge katika Majimbo ya Babati Mjini, Ukerewe, Simanjiro na Serengeti.
Akizungumza  ofisini kwake jijini Dar es Salaam, kuhusu uteuzi huo Kaimu Mkurugenzi wa Uchaguzi Giveness Aswile amesema kuwa,  wagombea  hao wanatoka katika vyama sita vya siasa ambavyo ni AFP, CCM, CUF, NCCR Mageuzi, NRA na UDP.
Amesema kuwa, hadi muda wa mwisho wa uteuzi Novemba 02, mwaka huu saa 10:00 jioni, jumla ya wagombea wane wa Ubunge kutoka CCM, waliteuliwa na hivyo kutangazwa kuwa wamepita bila kupingwa kwa mujibu wa kifungu cha 44 cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi.
Wagombea hao walitangazwa kupita bila kupinga baada ya wanachama wengine kutoka vyama vilivyochukua fomu za uteuzi, kukosa sifa kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo kushindwa kurudisha fomu hizo kwa wakati na wengine kutojaza fomu hizo kikamilifu ikiwa ni pamoja na kutojaza fomu ya kuheshimu na kuyazingatia maaadili ya uc... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More