VYAMA VYA MSINGI 35 VIMEHAKIKIWA NA VIPO TAYARI KULIPWA-HASUNGA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

VYAMA VYA MSINGI 35 VIMEHAKIKIWA NA VIPO TAYARI KULIPWA-HASUNGA

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii, Mtwara

WAZIRI wa Kilimo Japhet Hasunga, amesema serikali imeshaanza uhakiki wa wakulima wanaodai malipo ya korosho ambapo jumla ya vyama vya msingi 35 vimeshahakikiwa na malipo yameanza kufanyika.

Hayo aliyasema jana mkoani Mtwara wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu opereshe korosho inayoendelea katika mikoa inayolima korosho kuhakikisha wakulima wote wanauza korosho zao kwa serikali kwa bei ya Sh. 3,300.

"Tulitenga vyama 50 vya awamu ya kwanza na ndani ya siku mbili tumehakiki taarifa za wakulima kwenye vyama 35 kwa kuangalia majina yao, kiasi cha korosho walichoingiza kiasi cha fedha wanazotakiwa kulipwa na taarifa za akaunti zao na hivi ninavyoongea tayari wameanza kulipwa kuanzia sasa kupitia akaunti zao binafsi," alisema Hasunga.

Alitaja halmashauri ambazo vyama vyao vimehakikiwa kuwa ni pamoja na Halmashauri ya Newala (5) Wilaya ya Newala (5) Wilaya ya Masasi (5) Nanyumbu (2) Lindi (5) Tunduru Ruvuma (5).Kuhusu malipo ya ki... Continue reading ->
Source: Issa MichuziRead More