VYAMA VYA UKOMBOZI BARANI AFRIKA VYATAKIWA KUINGIA KATIKA AWAMU YA PILI YA UKOMBOZI WA KIUCHUMI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

VYAMA VYA UKOMBOZI BARANI AFRIKA VYATAKIWA KUINGIA KATIKA AWAMU YA PILI YA UKOMBOZI WA KIUCHUMI

Na Said Mwishehe, Globu ya jamiiVYAMA vilivyoshiriki kupigania ukombozi wa Bara la Afrika sasa vimetakiwa kuingia awamu ya pili ya ukombozi wa kiuchumi kwa ajili ya maendeleo ya Bara la Afrika huku vikitakiwa kukomesha rushwa, ufisadi na ubadhirifu.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Balozi Seif Ali Idd wakati anafunga mkutano wa siku mbili uliohusisha vyama vilivyokuwa mstari wa mbele kupigania ukombozi Kusini mwa Bara la Afrika.
"Awamu ya kwanza ilikuwa ni kupigania uhuru kwa nchi za Afrika na sasa uhuru tunao, hivyo vyama hivyo vinatakiwa kuingia awamu ya pili ya ukombozi wa kiuchumi.
"Kuna kila sababu ya kujifunza kutoka China ambapo wameendesha mapinduzi ya kiuchumi na  kuwakomboa wananchi wake wapatao bilioni  mbili,"amesema.
Amefafanua kama si China mambo yangekuwa mabaya na kama ingekuwa inatolewa Kombe la Dunia kwa nchi ambayo imefanikiwa kujenga uchumi imara basi kombe lingekwenda China.
Balozi Idd amesema China imeku... Continue reading ->Source: Issa MichuziRead More