VYOMBO WA ULINZI NA USALAMA MKOANI VYATAKIWA KUENDELEZA USHIRIKIANO - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

VYOMBO WA ULINZI NA USALAMA MKOANI VYATAKIWA KUENDELEZA USHIRIKIANO

Na Tiganya VicentJESHI la Wananchi Tanzania (JWTZ) limetoa wito kwa vyombo vya ulinzi na usalama mkoani Tabora kufanyakazi kwa ushirikiano na uzalendo ili kuimarisha ulinzi wa eneo lao na nchi kwa ujumla.
Kauli hiyo imetolewa jana na Mkuu wa Kamandi ya Vikosi chini ya Makao Makuu ya Jeshi Meja Jenerali Sharif Othman wakati akizungumza na Wajumbe wa Kamati za Ulinzi na Usalama za Mkoa wa Tabora na zile za Wilaya zake wakati ziara yake ya kikazi mkoani humo.
Alisema ushirikiano utawasaidia kuwafanya kuwa kitu kimoja na kuwa nguvu ya pamoja katika kuhakikisha usalama na ulinzi wa wananchi na nchi kwa ujumla.
Meja Jenerali Othman alisema viongozi wa vyombo hivyo wanapaswa kujenga tabia ya kutembelea na kushirikiana katika shughuli mbalimbali kama vile michezo na sherehe kama sehemu ya kujenga mshikamano ambao ndio utawasaidia kuwa kitu kimoja katika ulinzi wa nchi.
Alisema hali hiyo itawasaidia kupeana taarifa kama kutakuwepo na jambo ambalo linahatarisha usalama wa nchi na hivyo kuchukua hatu... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More