VYUO VYA UALIMU VYAAGIZWA KUZALISHA WALIMU WA FIZIKIA WENGI-DKT SEMAKAFU - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

VYUO VYA UALIMU VYAAGIZWA KUZALISHA WALIMU WA FIZIKIA WENGI-DKT SEMAKAFU

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV

SERIKALI imesema kuwa walimu wa somo la Fizikia ni wachache na kutaka vyuo vya ualimu kuandaa walimu hao katika kwenda sambamba na malengo ya ya serikali.
Hayo ameseyasema Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolijia Dkt. Evamaria Semakafu wakati wa kufunga ya kuwa na mkutano wa Wadau wa Elimu ya Ualimu lililofanyika jijini Dar es salaam,amesema kuwa walimu wa hisabati na Kemia hakuna tatizo lilopo ni walimu wa somo la Fizikia.
Amesema kuwa serikali inafanya mikakati mbalimbali katika kuhakikisha suala elimu linakwenda kutokana na mdau kutambua nafasi yake kutekeleza sekta ya elimu nchini.
Dkt.Semakafu anasema kuwa serikali iko katika mchakato wa kuwa na bodi ya walimu ambao watakuwa wasimamizi maadili na weledi wa kufanya kazi hata ikitokea kuna ukiukaji wa weledi huo kuweza kuchukuliwa hatua.
“Kuwepo kwa bodi itaondoa wale wanaokiuka maadili kutoendelea na kazi kwani wengi wamekuwa wakiuka na wakati mwingine anakwenda kuajiriwa sehemu nyingine... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More