WAAJIRI WASHAURIWA KUTOA MAFUNZO KWA VIONGOZI WAPYA WA MABARAZA YA WAFANYAKAZI SERIKALINI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WAAJIRI WASHAURIWA KUTOA MAFUNZO KWA VIONGOZI WAPYA WA MABARAZA YA WAFANYAKAZI SERIKALINI

Waajiri katika Wizara, Idara Zinazojitegemea, Wakala, Mamlaka za Serikali za Mitaa na Sekretarieti za mikoa wametakiwa kutoa mafunzo kwa wajumbe na viongozi wapya wa mabaraza ya wafanyakazi ili waweze kumudu majukumu yao ya kusimamia haki za watumishi ipasavyo.
Rai hiyo  imetolewa na Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Francis Michael wakati wa kikao cha baraza la wafanyakazi la ofisi yake kilichofanyika katika ukumbi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa jijini Dodoma.
Dkt. Michael amesema kuwa, endapo waajiri wataweka utaratibu wa kutoa mafunzo kwa viongozi na wajumbe wa mabaraza mapya ya wafanyakazi, itawawezesha kufahamu majukumu yao vizuri.“Wajumbe wa mabaraza ya wafanyakazi wakiingia kwenye mabaraza bila kujua majukumu na wajibu wao hawatawatendea haki wafanyakazi waliowachagua na kuwaamini kuwawakilisha kwenye mabaraza hayo” Dkt. Michael amesema.
Dkt. Michael ameongeza kuwa, mafunzo kwa viongozi na wajumbe wa mabaraza ya... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More