Waandishi wa habari Uganda kuishtaki mamlaka ya mawasiliano wa nchi hiyo, ni baada ya kuagizwa wasimamishwe kazi - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Waandishi wa habari Uganda kuishtaki mamlaka ya mawasiliano wa nchi hiyo, ni baada ya kuagizwa wasimamishwe kazi

Waandishi habari katika kampuni 13 za vyombo vya habari Uganda, walioagizwa wasitishwe kazi na mamlaka ya mawasiliano nchini, wanawasilisha kesi kesho Jumatano kupinga agizo hilo.


Uganda Journalists


Mamlaka ya mawasiliano Uganda (UCC) iliziambia kampuni hizo zichukue hatua dhidi ya baadhi ya wasimamizi, na wakuu wa vipindi kufuatia tuhuma kwamba wamekiuka maadili ya utangazaji katika kuangazia matukio yanayomhusu Bobi Wine, mwanasiasa wa upinzani na mkosoaji wa serikali.


Kesi hiyo inaotazamwa kama mtihani mkubwa kwa uhuru wa vyombo vya habari nchini Uganda.


Kwa mujibu wa shirika la habari la BBC, Waandishi kadhaa wa habari wamepewa majukumu mbadala ya muda kwa mwezi ila hawakusimamishwa kazi, kukisubiriwa matokeo ya kesi hiyo.


Katika mkutano wiki iliyopita na wamiliki vyombo vya habari, mkurugenzi mtendaji wa tume hiyo ya mawasiliano, Godfrey Mutabazi, aliridhia kwamba waandishi waliotuhumiwa wakae kando wakati wa uchunguzi kubaini iwapo “tabia ya mtu” “iliambatana na kilichokuwa kinatangazwa hewa... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More