WABUNGE KUOSHA MAGARI KUCHANGIA UJENZI WA VYOO NCHINI JUNI 8, 2018 - Kajunason | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WABUNGE KUOSHA MAGARI KUCHANGIA UJENZI WA VYOO NCHINI JUNI 8, 2018

Mwandishi Wetu, Dodoma.
Wabunge wakiongozwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai wanatarajia kuosha magari ili kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa vyoo vya mfano kwa watoto wa kike na wenye uhitaji maalumu.
Tukio hilo litakalofanyika kesho Jumamosi Juni 8, katika Uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma, limeandaliwa na Spika Ndugai ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono jitihada za Umoja wa Wabunge Wanawake (TWPG), katika kampeni yao ya ujenzi wa vyoo hivyo, litahusisha uoshaji magari ya wabunge na watu mbalimbali.
Hata hivyo, tukio hili ni utangulizi wa harambee iliyoandaliwa na TWPG, itakayofanyika Juni 22 mwaka huu, jijini Dodoma ili kuchangisha fedha za kujenga vyoo vya kisasa katika majimbo yote nchi nzima ili kumkomboa mtoto wa kike apate mahitaji muhimu na kwa utulivu, ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais John Magufuli.
Akizungumzia tukio la kesho, Spika Ndugai amewataka watu mbalimbali kujitokeza kuosha magari yao ili kuchangisha fedha za ujenzi wa vyoo hivyo.
“Natoa wito kwa wote wenye magari,... Continue reading ->
Source: KajunasonRead More