Wabunge waombwa kuunga mkono kazi za wasaidizi wa kisheria - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Wabunge waombwa kuunga mkono kazi za wasaidizi wa kisheria

Meneja Mradi Legal Services Facility, Ramadhan Masele, akiongea na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba (hawapo pichani) jijini Dodoma.
Na Mwandishi Wetu
Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wameombwa kuunga mkono kazi za wasaidizi wa kisheria na watoa huduma za msaada wa kisheria nchini baada ya huduma zao kuonekana zikiwasaidia mamilioni ya Watanzania kuondokana na vitendo vya kikatili na udhalimu.
“Ni kweli kwamba wasaidizi wa kisheria na watoa huduma za msaada wa kisheria wengine wamekuwa msaada mkubwa kwa makundi mbalimbali ya watu wanaoishi kwenye mazingira magumu na wanaoweza kudhurika, lakini hawawezi kutoa huduma bila ya kusaidiwa kama ambavyo wabunge nao hawawezi kufanya kazi kwa ufanisi bila msaada wa watu wengine,” alisema Ramadhan Masele, ambaye ni meneja wa mpango wa Taasisi ya Msaada wa Kisheria (LSF) wakati wa ufunguzi wa semina ya mafunzo ya siku mbili kwa wabunge juu ya wasaidizi wa kisheria na watoa huduma za kisheria nchini. LSF, ambayo ni... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More