WACHEZAJI WA TIMU YA SIMBA WAFANYA UCHUNGUZI WA MAGONJWA YA MOYO KATIKA TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE (JKCI) - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WACHEZAJI WA TIMU YA SIMBA WAFANYA UCHUNGUZI WA MAGONJWA YA MOYO KATIKA TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE (JKCI)

 Na Brighton James
Vilabu vya mpira hapa nchini vimeshauriwa kupima afya za  wachezaji wao kabla ya kuanza kwa mashindano ili kama watakutwa na matatizo waweze kupata matibabu mapema.Rai hiyo imetolewa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi wakati akiongea na wachezaji wa Klabu ya Simba waliofika katika Taasisi hiyo kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa magonjwa ya moyo.Prof. Janabi alisema faida ya kufanya uchunguzi wa afya kutamsaidia  mchezaji kama atagundulika kuwa na matatizo ya moyo atapata matibabu mapema na kuepukana na kifo cha ghafla anachoweza kukipata awapo uwanjani.“Vifo vya wachezaji vinavyotokea ghafla wanapokuwa uwanjani vinaweza kuzuilika iwapi wangefanya uchunguzi wa afya zao mapema. Nazishauri timu zinazocheza ligi kuu pamoja na mashindano ya kitaifa na kimataifa wajitahidi kupima afya za wachezaji wao ikiwemo uchunguzi wa magonjwa ya moyo”, alisisitiza Prof. Janabi.Kwa upande wake Abasi Ally ambaye ni Mkuu wa msafara kutoka klabu ya Simba alisema wameamua kuwafanyia wachezaji wao uchunguzi wa magonjwa ya moyo  kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi kuu ya Tanzania inayotarajia kuanza mwishoni mwa mwezi ujao.Ally alisema kwamba kuwapima afya wachezaji hao kutawasaidia kujuwa afya zao ili kama mchezaji atakutwa na matatizo aweze kupata matibabu mapema na kushiriki mashindano akiwa na afya njema.Jumla ya wachezaji 27 wa klabu hiyo wamefanyiwa uchunguzi wa magonjwa ya moyo kwa kuangaliwa jinsi mioyo yao inavyofanya kazi (ECHO), umeme wa  moyo (ECG) na  umeme wa moyo wakati mtu anafanya mazoezi (Stress ECG) Mfanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Abuu Dalidali akimpima urefu Mchezaji  wa Klabu ya Simba Yussuf Mlipili wakati wachezaji wa timu hiyo walipofika katika Taasisi hiyo leo kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa magonjwa ya moyo. 
 Muhudumu wa Afya wa  Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Seleman Charles akimpima urefu Shiza Ramadhani Kichuya ambaye ni Mchezaji  wa Klabu ya Simba wakati wachezaji wa timu hiyo walipofika katika Taasisi hiyo leo kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa magonjwa ya moyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akisimamia  upimaji wa magonjwa ya moyo ulivyokuwa unafanyanyika kwa wachezaji wa klabu ya Simba wakati wachezaji wa timu hiyo walipofika katika Taasisi hiyo leo kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi.Picha na JKCI


Source: Issa MichuziRead More