Wachezaji waikimbia Stand United - Shaffih Dauda | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Wachezaji waikimbia Stand United

Uongozi wa Stand United umekiri kuwa katika wakati mgumu baada ya kuondokewa na nyota wao wote wa kimataifa raia wa Burundi ambao hawakurejea kikosini baada ya kupewa ruhusa ya kwenda kwenye majukumu ya timu ya taifa na kuifanya timu kubakiwa na wachezaji 20 pekee.


Meneja wa Stand United Fred Masai amesema wameamua kupandisha wachezaji toka timu ya vijana katikati ya msimu kuokoa jahazi.


“Tumepata changamoto baada ya wachezaji wengi kuondoka kwenye kikosi lakini tumepandisha wachezaji wengine kutoka timu ya vijana wanajitahidi kufanya vizuri.”


“Wachezaji wote wa kigeni tuliowasajili wametuangusha sana tuliwapa ruhusa lakini wameshindwa kurudi na hawana sababu za msingi na kwa sababu ni wachezaji ambao wapo nchi nyingine tunalazimika kubaki na wazawa.”


“Tumekuwa na kikosi kidogo (wachezaji 20) kwa hiyo wachezaji wanaotumika ni walewale unakuta mchezaji anaharibu lakini unatakiwa kumtumia huyohuyo.”


Meneja wa Stand anasema wachezaji wakigeni walikuwa wanadai mshahara wa mwezi... Continue reading ->


Source: Shaffih DaudaRead More