WACHUNGAJI WAMUOMBEA MAKONDA KUMLINDA NA MAADUI - Kajunason | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WACHUNGAJI WAMUOMBEA MAKONDA KUMLINDA NA MAADUI

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, akifanyiwa maombi.
Mchungaji Kiongozi Dk Getrude Lwakatare almaarufu Mama Lwakatare wa Kanisa la Mlima wa Moto Assemblies of God la Mikocheni B jijini Dar na wachungaji wenzake, usiku wa kuamkia jana, waliguswa na uongozi wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kisha kumuombea ili kumuimarisha katika uongozi wake na kumkinga na maadui. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, akizungumza jambo.
Tukio hilo lilijiri kanisani hapo ambapo mama Lwakatare alimwita mbele Makonda kisha kuwaita wachungaji wenzake na kumfanyia maombi hayo.Maombi maalum yakiendelea.
Baada ya kumwita mbele, Mama Lwakatare na kanisa lote lilimwangushia maombi mazito Makonda kutokana na kazi ngumu anayoifanya katika jamii kama kupambana na madawa ya kulevya, rushwa, kusaidia kina mama na watoto waliotelekezwa na mengine mengi.
Tukio hilo lilijiri kwenye usiku wa wanandoa ambapo waimbaji kama Bahati Bukuku na Christina Shusho walipamba kwa burudani ya nyimbo za Inji... Continue reading ->


Source: KajunasonRead More