WADAU WA HABARI WAOMBA KUKUTANA NA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI (NEC) - Kajunason | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WADAU WA HABARI WAOMBA KUKUTANA NA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI (NEC)

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG


Wadau wa habari kutoka taasisi na vyombo mbalimbali vya habari nchini wameomba kukutana na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), ili kuimarisha mahusiano mema wakati ambao taifa linaelekea kwenye uchaguzi mdogo mwaka huu pamoja na uchaguzi mkuu hapo mwakani.


Pamoja na mambo mengine, wadau hao waliazimia hilo juzi kwenye warsha ya kuwajengea uwezo viongozi wa vyombo vya habari ili kuangalia na kuripoti kwa weledi habari za uchaguzi, iliyofanyika jijini Dodoma kwa siku tatu kuanzia Aprili 15, 2019 ikiandaliwa na taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania kwa kushirikiana na Ubalozi wa Marekani.


Akisisitiza hilo, Mkurugenzi wa Mawasiliano kutoka taasisi ya Internews, Wenceslaus Mushi alisema wadau wa habari pamoja na maafisa kutoka NEC ni vyema wakakutana kwenye warsha ya pamoja na kujengeana weledi namna kila upande unaweza kutimiza majukumu yake kwa mujibu wa sheria katika kipindi cha uchaguzi na hivyo kuondoa mkanganyiko ambao wakati m... Continue reading ->


Source: KajunasonRead More