WADAU WAKUTANA TABORA KUANDAA JUMBE ZA KUTOKOMEZA UKATILI WA WANAWAKE NA WATOTO - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WADAU WAKUTANA TABORA KUANDAA JUMBE ZA KUTOKOMEZA UKATILI WA WANAWAKE NA WATOTO

WANANCHI wametakiwa kuunganisha nguvu pamoja kuhakikisha wanatokemeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto na mimba za utotoni hapa nchini kama ilivyoekelezwa katika Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokemeza Ukatili wa wanawake na watoto(MTAKUWWA). Tatizo hilo linasababisha athari nyingi ikiwemo vifo, ulemavu , kuwa na kundi kubwa la watoto kukimbilia mitaani na umaskini kwa watoto wanaokatishwa masomo na ndoto zao la baadae na hivyo kudhofisha juhudi za ujenzi wa uchumi wa kati na viwanda hapa nchini.
Kauli hiyo imetolewa  na Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu katika hotuba yake iliyosomwa na Katibu Tawala Msaidizi Raphael Nyanda kwenye ufunguzi wa mafunzo ya kuandaa ujumbe wa kupinga ukatili dhidi ya wananwake na watoto na mimba za utotoni. Alisema suala hilo ni kubwa katika baadhi ya jamii na hivyo linahitaji kila mwanajamii kuwa mstari wa mbele kukemea na kutoa taarifa ambazo zitasaidia kukomesha ukatili kwa watoto , wanawake na kuondoa ndoa na mimba za utotoni hapa nchini na wah... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More