WADAU WAOMBWA KUJITOKEZA KUSAIDIA MAANDALIZI YA MASHINDANO YA SOKA KWA WENYE ULEMAVU AFRIKA MASHARIKI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WADAU WAOMBWA KUJITOKEZA KUSAIDIA MAANDALIZI YA MASHINDANO YA SOKA KWA WENYE ULEMAVU AFRIKA MASHARIKI

Na Nyamagory Omary, PMOWizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu imewataka wapenzi na wadau wa soka nchini kushiriki  maandalizi ya mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu kwa watu wenye ulemavu Afrika Mashariki (CECAAF) yanayotarajiwa kufanyika nchini Mwishoni mwa mwezi Juni mwaka huu.Akizungumza  na waandishi wa habari  leo Mei 16, 2019 Jijini Dodoma,katika mkutano uliolenga kuitambulisha kamati ya wabunge watano waliojitolea kuhamasisha Watanzania,kushiriki kwa hali na mali katika mashindano hayo,  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe, amesema kuwa mashindano hayo yatashirikisha nchi za Tanzania Bara, Zanzibar, Uganda, Kenya na Rwanda.“Mashindano haya yatakayokuwa ya kwanza kufanyika katika ukanda huu wa Afrika yameanzishwa kwa mujibu wa mkataba wa Umoja wa Mataifa wa haki za Walemavu wa mwaka 2006, unaotaka haki ya Walemavu kushiriki katika mambo kadhaa ikiwemo michezo”Akifafanua zaidi, Dkt. Mwakye... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More