WAFANYABIASHARA MKOANI SONGWE WATAKIWA KUJITOKEZA KWA WINGI KUPATIWA HUDUMA YA NAMBA YA UTAMBULISHO YA MLIPAKODI INAYOAMBATANA NA ELIMU YA KODI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WAFANYABIASHARA MKOANI SONGWE WATAKIWA KUJITOKEZA KWA WINGI KUPATIWA HUDUMA YA NAMBA YA UTAMBULISHO YA MLIPAKODI INAYOAMBATANA NA ELIMU YA KODI


Na. Benedict Liwenga-TRA. 
WAFANYABIASHARA Mkoani Songwe wametakiwa kujitokeza kwa katika Kampeni ya Usajili na Elimu kwa Mlipakodi inayoendeshwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). 
Kauli hiyo imetolewa leo na Afisa Kiongozi wa Kituo cha Huduma cha TRA mjini Tunduma wakati wa Kampeni ya Usajili na Elimu kwa Walipakodi mkoani hapo ambapo amewataka Wafanyabiashara kujitokeza kwa wingi kuweza kupatiwa huduma hiyo pasipo gharama yoyote. 
Bwana Mwita ameeleza kuwa, mwitikio wa wafanyabiashara katika kampeni hiyo ni mkubwa, ambapo wengi wa Wafanyabiashara ambao walikuwa hawana Namba ya Utambulisho ya Mlipakodi (TIN) wameshasajiliwa na kupatiwa TIN hizo. 
“Zoezi hili ni zuri na mwitikio wa watu ni mkubwa, niwaombe Wafanyabiashara waendelee kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kupatiwa TIN na elimu kuhusu masuala ya kodi”, alisema Mwita. 
Kwa upande wake Kiongozi wa msafara kutoka TRA Makao Makuu ambaye pia ni Afisa Mkuu Mwandamizi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi, Bi. Rose Mahendeka amesem... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More