Wafanyabiashara wajazwa mamilioni kwa kufanya miamala - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Wafanyabiashara wajazwa mamilioni kwa kufanya miamala

Kampuni ya Selcom kwa kushirikiana na Mastercard imetoa zawadi ya Sh milioni tatu kwa wafanyabiashara wanaotumia huduma ya Masterpass QR katika kupokea malipo mbalimbali kwenye maeneo yao ya biashara. 
Zawadi hizo zimetolewa jana katika promosheni ya “Shinda Mtaji” iliyoanza rasmi Novemba mwaka huu kwa lengo la kuwarahisishia wafanyabiashara hao kutumia huduma ya Masterpass QR kufanya miamala mbalimbali. 
Akizungumza promosheni hiyo, Meneja Masoko wa Selcom, Juma Mgori alisema promosheni hii inamuwezesha mfanyabiashara kujishindia Sh milioni moja kila wiki kwa muda wa miezi mitatu kuanzia Novemba mwaka huu hadi Januari mwaka 2019. 
Aidha, aliwataja wateja walioshinda milioni moja kila mmoja kuwa ni Boaz Wales, Hamisi Kilenga wote wa mkoani Dar es Salaam na mfanyabiashara mmoja kutoka Arusha. 
Alisema kila mfanyabiashara atakayejiunga na Masterpass QR na kuanza kupokea miamala kutoka kwa wateja, ataingia moja kwa moja kwenye droo ya promosheni kwa wiki hiyo na kupata nafasi ya kujis... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More