WAFANYABIASHARA WATAKIWA KUTUMIA MAWAKALA WALIOTHIBITISHWA NA TRA KUPATA KARATASI ZA RISITI - Kajunason | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WAFANYABIASHARA WATAKIWA KUTUMIA MAWAKALA WALIOTHIBITISHWA NA TRA KUPATA KARATASI ZA RISITI

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb)
Serikali imetatua tatizo la kuwepo kwa karatasi za risiti zinazofutika maandishi zinazotolewa na Mashine za Kielektroniki za kutolea Risiti (EFDs) kwa kuwataka wafanyabiashara wote kununua karatasi hizo kwa mawakala waliothibitishwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Hayo yameelezwa Bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Tanga Mjini Mhe. Mussa Bakari Mbarouk, aliyetaka kujua kauli ya Serikali kuhusu risiti zinazotolewa na Mashine za EFDs kufutika maandishi kwa muda mfupi na muda ambao utatolewa kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kurekebisha hali hiyo.
Akijibu swali hilo Dkt. Kijaji alieleza kuwa Serikali inatambua kuwa kuna karatasi feki, lakini tatizo la kufutika kwa risiti halihitaji kutoa muda kwa TRA wa kufanya marekebisho kwa kuwa Serikali ililifanyia kazi, hivyo ni jukumu la wafanyabiashara kufuata maelekezo ya ununuzi wa k... Continue reading ->


Source: KajunasonRead More