Wafanyakazi wa TAA wapigwa msasa na KOICA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Wafanyakazi wa TAA wapigwa msasa na KOICA

Watendaji wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) kutoka Menejimenti na Vitengo vya Usalama, na uzuiaji wa wanyama pori na ndege hai  leo wameshiriki katika mafunzo  ya kuwajengea uwezo wa utendaji katika Viwanja vya Ndege yaliyoandaliwa na KOICA (Korea International Cooperation Agency)  na kutekelezwa na wataalam kutoka Kiwanja cha Ndege cha Incheon kilichopo Korea Kusini ambacho kinaaminika kuwa na ubora nambari moja katika nyanja ya usalama na uendeshaji duniani.
Mafunzo hayo yamefanyika katika Ukumbi wa watu mashuhuri Katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere Jengo la pili la abiria (TB II), ikiwa ni  mwendelezo wa mpango wa mafunzo ya miaka mitatu kwa watendaji wa TAA na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar (ZAA).Akitoa maelezo kuhusu mafunzo hayo Meneja wa Mafunzo kutoka Kiwanja cha Ndege cha Incheon Bi. Ji-Yoon Park ameeleza kwamba mafunzo hayo ni mwendelezo wa mafunzo ya awali ambapo kwa awamu ya kwanza Mafunzo yalitolewa kwa watendaji takribani 15 ku... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More