WAFANYAKAZI WATANO NEMC WAPATA DHAMANA KESI YA UHUJUMU UCHUMI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WAFANYAKAZI WATANO NEMC WAPATA DHAMANA KESI YA UHUJUMU UCHUMI

Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii
WAFANYAKAZI watano wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) wamefanikiwa kupata dhamana baada ya Mahakama Kuu Kitengo cha Uhujumu Uchumi kuridhia wapate dhamana na kuwapangia masharti ya dhamana.
Hatua hiyo imekuja baada ya washtakiwa kupitia mawakili wao kupeleka maombi ya dhamana Mahakama Kuu kwa kuwa washtakiwa wameshtakiwa chini ya sheria ya Uhujumu Uchumi ambapo kesi hizo zinasikilizwa Mahakama Kuu.
Washtakiwa waliopata dhamana ni Ofisa wa Mazingira NEMC, Deusdith Katwale(38) na Mtaalam wa IT NEMC, Luciana Lawi(33) wote wakazi wa Ubungo Msewe, Katibu Muhasi wa NEMC (Sekretari), Edna Lutanjuka (51) Mkazi wa Mbezi Beach St Gasper, Msaidizi wa ofisa Mwaruka Mwaruka (42) na Ofisa mazingira Nemc, Lilian Laizer (27) wote wakazi wa Ukonga Mombasa.
Washitakiwa hao Octoba31, Mwaka huu walisomewa mashtaka sita ya uhujumu uchumi likiwamo la kughushi saini ya Waziri wa Nchi,Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Januari Makamba... Continue reading ->Source: Issa MichuziRead More