wafanyakazi watatu wa Kampuni ya Jiangxi Internatiol wahukumiwa kutumikia kifungo cha miaka 2 jela ama kulipa faini ya Milioni 9.3 - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

wafanyakazi watatu wa Kampuni ya Jiangxi Internatiol wahukumiwa kutumikia kifungo cha miaka 2 jela ama kulipa faini ya Milioni 9.3

 Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imewahukumu kutumikia kifungo cha miaka 2 jela ama kulipa faini ya Milioni 9.3 wafanyakazi watatu wa Kampuni ya Jiangxi Internatiol (T) Investment Ltd baada ya kukiri makosa ya kushindwa kuchukua tathmini ya uaribifu wa mazingira.
Washtakiwa hao ni Injinia Xia Yanan (26), Chen Jinchuan (31) raia wa China  na Mtala Habibu (29) fundi umeme raia wa Tanzania.
Hukumu hiyo imetolewa leo Novemba 7.2018 na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi baada ya Wakili wa Serikali Nassoro Katuga kuwasomea washtakiwa makosa yao na kukiri.
Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Shaidi amesema kutokana na washtakiwa kukiri makosa yao anawahukumu kila mmoja kulipa faini ya Shilingi Milioni Tatu na laki moja kwa makosa yote mawili ama kwenda kutumikia kifungo cha miaka miaka 2 gerezani.

Amesema katika kosa la kwanza la kushindwa kuchukua tathmini ya uaribifu wa mazingira,  anawahukumiwa washtakiwa kila mmpja kulipa faini ya Shilingi Milioni 3 ama kwenda jela... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More