WAFANYAKAZI WAWILI WA TBS WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUSABABISHA HASARA ZAIDI YA MIL 977 - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

WAFANYAKAZI WAWILI WA TBS WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUSABABISHA HASARA ZAIDI YA MIL 977

Na Karama Kenyunko, blogu ya Jamii.AFISA  Manunuzi  Mwandamizi wa Hifadhi ya Taifa ya Chakula, Mohamedx Mzingi na Mkuu wa Textile Leather wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na makosa miwili likiwemo la matumizi mabaya ya madaraka na kusababisha hasara ya zaidi ya Sh milioni 977.Akisoma hati mashtaka wakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Aneth Mavika amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Augustina Mmbando kuwa kati ya Julai 16 na 30, mwaka 2013 katika ofisi za Makao Makuu ya Hifadhi ya Chakula (NFRA) washtakiwa walitenda kosa.
Imedaiwa siku ya tukio washtakiwa hao kwa nafasi zao na wakiwa wajumbe wa uthamini wa zabuni walitumia madaraka yao vibaya katika uthamini wa  zabuni namba AE-054/2013/2014/HQ/G/02 Lot namba 01.
Wakili huyo aliendelea kudai kuwa washtakiwa walitenda kosa hilo wakati wakitekeleza majukumu yao ambapo kwa makusudi walipendekeza kampuni ya Bajuka International (T) Ltd ambayo ilikuwa ha... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More